IJUE BIBLIA - Sehemu ya I
UTANGULIZI
Biblia ni nini?
Biblia
ni mkusanyiko wa vitabu 66 vilivyo andikwa na waandishi tofauti-tofauti 40 kwa
takribani miaka 1500. Waandishi walikuwa wafalme, wavuvi, makuhani, viongozi wa
serikali, wakulima, wachungaji, na madaktari. Biblia ni kitabu cha ajabu!
Pamoja na kwamba vitabu vyake vimeandikwa na waandishi wengi tena kwa muda
mrefu sana, bado kuna mtiririko na muunganiko wa ajabu kuanzia kitabu cha
kwanza hadi cha mwisho. Hivyo basi kwa ujumla wake Biblia imeandikwa na wanadamu
chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu wa Mungu
“Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko
upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote
kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinenayaliyotoka kwa Mungu,
wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” (2 Petro 1: 20, 21)
MGAWANYIKO WA BIBLIA
Utangulizi
Biblia imegawanyika
katika sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza inaitwa agano la kale lenye jumla ya
vitabu 39 na sehemu ya pili inaitwa agano jipya lenye jumla ya vitabu 27. Kisha
ikagawanyika katika sehemu nane; nne za agano la kale na nne za agano jipya.
Yesu Kristo ndiye mzungumzwaji mkuu katika biblia nzima. Huonekana kama
Mwokozi, tumaini la kweli kwa wanadamu wote. Yeye mwenyewe (Yesu Kristo)
alishuhudia kuwa ndiye mhusika (mzungumzwaji)
mkuu katika agano jipya
- Katika Mathayo 5: 17, 18 alisema, “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka, hata yote yatimie.”
- Alipokuwa akitembea na wanafunzi wake kuelekea Emau baada ya kufufuka, Luka 24: 13-31 inasema “ ... Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe...
- Kisha baadaye jioni alipokuwa akizungumza na wanafunzi wake aliwaambia “... hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.”
- Katika Yohana 5:39 na 40, wakati Yesu anazungumza na Wayahudi alisema “Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndaniyake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima”
Zaidi sana, katika
Ufunuo 19:10 biblia inasema “... kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya
unabii” Kwa maneno mengine, asili na kusudi halisi la unabii na maandiko yote
ni kumtangaza au kumdhihirisha Yesu Kristo. Anguko na uhitaji wa wokovu kwa
mwanadamu, hasa ndivyo vinavyo changia Kisto Yesu kudhihirishwa and kutangazwa
kwenye maandiko ya Agano la Kale na Agano Jipya. Kupitia Yesu Kristo tunapata
uzima wa milele (Yohana 10:10)
Agano la Kale
Agano la kale lina
jumla ya vitabu 39 ambavyo vimegawanyika katika makundi makuu manne kama
ifuatavyo:
NO.
|
MGAWANYIKO WA AGANO LA KALE (A.K)
|
NO.
|
VITABU HUSIKA NDANI YA MGAWANYIKO WA A.K
|
1.
|
Vitabu vya Sheria
|
1.
|
Mwanzo
|
2.
|
Kutoka
|
||
3.
|
Mambo ya Walawi
|
||
4.
|
Hesabu
|
||
5.
|
Kumbukumbu la Torati
|
||
2.
|
Vitabu vya Kihistoria
|
1.
|
Joshua
|
2.
|
Waamuzi
|
||
3.
|
Ruthu
|
||
4.
|
1 Samweli
|
||
5.
|
2 Samweli
|
||
6.
|
1 Wafalme
|
||
7.
|
2 Wafalme
|
||
8.
|
1 Mambo ya Nyakati
|
||
9.
|
2 Mambo ya Nyakati
|
||
10.
|
Ezra
|
||
11.
|
Nehemia
|
||
12.
|
Esta
|
||
3.
|
Vitabu vya Kiushairi
|
1.
|
Ayubu
|
2.
|
Zaburi
|
||
3.
|
Mithali
|
||
4.
|
Muhubiri
|
||
4.
|
Vitabu vya Manabii
|
||
a)
Vitabu vya Manabii Wakubwa
|
1.
|
Isaya
|
|
2.
|
Yeremia
|
||
3.
|
Ezekiel
|
||
4.
|
Danieli
|
||
b)
Vitabu vya Manabii Wadogo
|
1.
|
Hosea
|
|
2.
|
Yoeli
|
||
3.
|
Amosi
|
||
4.
|
Obadia
|
||
5.
|
Yona
|
||
6.
|
Mika
|
||
7.
|
Nahumu
|
||
8.
|
Habakuki
|
||
9.
|
Zefania
|
||
10.
|
Hagai
|
||
11.
|
Zekaria
|
||
12.
|
Malaki
|
||
Agano la Jipya
Agano jipya lina
jumla ya vitabu 27 ambavyo vimegawanyika katika makundi makuu manne kama
ifuatavyo:
NO.
|
MGAWANYIKO WA AGANO LA JIPYA (A.J)
|
NO.
|
VITABU HUSIKA NDANI YA MGAWANYIKO WA A.J
|
1.
|
Vitabu vya Kihistoria
|
1.
|
Mathayo
|
2.
|
Marko
|
||
3.
|
Luka
|
||
4.
|
Yohana
|
||
5.
|
Matendo Ya Mitume
|
||
2.
|
Nyaraka za Mtume Paulo
|
1.
|
Warumi
|
2.
|
1 Wakorintho
|
||
3.
|
2 Wakorintho
|
||
4.
|
Wagalatia
|
||
5.
|
Waefeso
|
||
6.
|
Wafilipi
|
||
7.
|
Wakolosai
|
||
8.
|
1 Wathesalonike
|
||
9.
|
2 Wathesalonike
|
||
10.
|
1 Timotheo
|
||
11.
|
2 Timotheo
|
||
12.
|
Tito
|
||
13.
|
Filemoni
|
||
3.
|
Nyaraka za Jumla (kwa watu wote)
|
1.
|
Waebrania
|
2.
|
Yakobo
|
||
3.
|
1 Petro
|
||
4.
|
2 Petro
|
||
5.
|
1 Yohana
|
||
6.
|
2 Yohana
|
||
7.
|
3 Yohana
|
||
8.
|
Yuda
|
||
4.
|
Kitabu cha Unabii
|
1.
|
Ufunuo wa Yohana
|
Endelea kufuatilia somo linalofuata kwa
uchambuzi wa kina. Share kwenye mitandao ya kijamii ili watu wapete nafasi ya
kujifunza kama wewe ulivyojifunza.
Maoni
Chapisha Maoni