HIVI NDIVYO MTU ANAVYOOKOKA
Biblia husema ... “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka . Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. ” [Warumi 10: 9,10] Ili mtu aokoke alizima... 1. Kuamini moyoni kuwa Mungu alimfufua Yesu katika wafu. Hii ina maana ya kuamini kazi nzima ya ukombozi wa mwanadamu ambayo Yesu Kristo aliikamilisha baada ya kufa msalabani na kufufuka siku ya tatu. Unapofika mahali pa kuyaangalia maisha yako na kuona kweli unamhitaji Yesu, basi hapo unapaswa kwanza kuamini kuwa Yesu alikufa msalabani kwa ajili yako ili upate msamaha wa dhambi. Biblia husema.....